Qur-aan, Sunnah na mfumo wa Salaf – silaha nzito dhidi ya kila upotevu

Swali: Je, inajuzu kutaamiliana na makundi na mapote yaliyopo ambayo yanasifiwa ya kwamba ni yenye kupindukia na ni ya kigaidi kama mfano wa Tabliygh na al-Ikhwaan katika kulingania?

Jibu: Fuateni njia ya as-Salaf as-Swaalih na mfumo wa Salaf wa Ummah na maimamu wao. Mfumo wao uko wazi na umesimama imara. Fuateni mfumo huu. Jiungeni nao. Hivyo Allaah atakulindeni – kwa idhini Yake – kutokamana na kila upotevu, kila utata na kila upumbavu. Ni mfumo wa wazi. Shikamaneni nao. Hivyo ndivyo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mimi nimekuachieni yale ambayo endapo mtashikamana nayo basi hamtopotea kamwe baada yangu; Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu.”

Qur-aan na Sunnah viko mbele yetu na vimehifadhiwa. Kwa hiyo mbele yetu tuko na silaha dhidi ya kila batili, dhidi ya kila utata, dhidi ya kila Bid´ah na dhidi ya kila upotevu. Tuko na silaha zenye kuangamiza batili hizi na himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17754
  • Imechapishwa: 11/04/2018