1962- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakitoacha kikundi kutoka katika Ummah wangu kuwa ni chenye kunyooka juu ya amri ya Allaah na hakitodhurika na wale wenye kwenda kinyume nao.”

Ameipokea Ibn Maajah (1/7) kupitia kwa Abu ´Alqamah Naswr bin ´Alqamah, kutoka kwa ´Umayr bin al-Aswad na Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Cheni ya wapokezi ni nzuri – Allaah akitaka. Wapokezi wake ni wanaume wa Swahiyh isipokuwa tu Naswr bin ´Alqamah ambaye amefanywa kuwa ni mwaminifu. Katika ”at-Taqriyb” ameelezwa kwamba ni mwenye kukubaliwa. Hadiyth imepokelewa kwa njia nyingine ambayo imekuja kwa tamko lisemalo:

”Hawatoacha kuendelea kuwa juu ya jambo hili… ”

Mwanzoni (270) nilitaja kwamba vyanzo vya Hadiyth na kuihukumu na nikathibitisha kwamba Hadiyth imepokelewa na Maswahabah nane. Nimeitaja Hadiyth kwa ufupi wake pasi na kutaja matini na matamshi yake. Lengo langu ilikuwa kumjuza msomaji yale yanayosemwa na wanachuoni na maimamu kuhusu kundi lililonusuriwa na kwamba wao ni Ahl-ul-Hadiyth. Hivi sasa nitajishughulisha na kutaja vyanzo vya Hadiyth na kuihukumu na matamshi yake mbalimbali ili kubainisha faida zake ambazo haziwezi kufikiwa kwa njia nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (4/604)
  • Imechapishwa: 22/05/2019