Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika picha kwenye ukuta?

Jibu: Kutundika picha kwenye ukuta, khaswa wale wakuu, ni haramu. Haijalishi kitu kama ni sehemu ya kiwiliwili na kichwa. Ni dhahiri kwamba makusudio ni maadhimisho. Msingi wa shirki ni upetukaji huu kama ilivyopokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia pickuhusu masanamu ya watu wa Nuuh (´alayhis-Salaam) yanayoabudiwa ya kwamba yalikuwa ni majina ya wanaume wema ambao zilitengenezwa sura zao ili yaweze kuwakumbusha ´ibaadah. Baada ya kupita muda wakayaabudu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/282)
  • Imechapishwa: 04/06/2017