Pepo na Moto tayari vimeshaumbwa na Moto wameandaliwa makafiri

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ

“Mkiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu, basi leteni Suurah mfano wake na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. Msipofanya na wala hamtoweza kufanya, basi uogopeni Moto ambao mafuta yake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa ajili ya makafiri.”[1]

Maneno Yake

أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ

“… umeandaliwa kwa ajili ya makafiri.”

na Aayah nyenginezo mfano wake ni dalili juu ya madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwamba Pepo na Moto tayari vimekwishaumbwa. Tofauti na vile wanavoona Mu´tazilah.

Jengine ni kwamba muislamu mtenda dhambi kubwa, ijapo atafanya baadhi ya dhambi kubwa, hatodumishwa Motoni milele. Kwa sababu amesema:

أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ

“… umeandaliwa kwa ajili ya makafiri.”

Lau ingelikuwa waislamu watenda dhambi kubwa watadumishwa Motoni milele, basi Moto usingealiandaliwa kwa ajili ya makafiri peke yao. Tofauti na vile wanavoona Khawaarij na Mu´tazilah.

Pia jengine ni kwamba kuna dalili ya kwamba adhabu inastahiki kutokana na sababu zake. Nazo ni ule ukafiri na aina mbalimbali za maasi kwa kutofautiana kwake.

[1] 02:23-24

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 21/05/2020