Swali: Je, atahadharishwe yule mwenye kusema kuwa maandamano yanafaa au ni katika mambo ya Ijtihaad?

Jibu: Maandamano hayajuzu kwa hali yoyote. Nyinyi wenyewe mmeona maandamano kwa macho yenu na mmeona yamepelekea katika kitu gani. Mmeona ni miji mingapi yameharibu na kuua watu. Yamefanya watoto kuwa mayatima na wanawake kuwa wajane. Yameangamiza nyumba na miji. Maandamano ni kitu kisichosilihi. Kutengeneza sio kwa kufanya maandamano. Kutengeneza kunakuwa kwa njia za Shari´ah zinazochukuliwa kuyafikia malengo. Haya yanakuwa kupitia mikono ya wanachuoni na watu wa maono na si kupitia kwa watu wa kawaida na wajinga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=135719
  • Imechapishwa: 20/03/2021