Nyimbo zisizokuwa na maadili harusini

Swali: Je, kupiga dufu zilizoko hivi sasa ndio jambo lililopendekezwa? Sunnah dufu hilo lipigwe na watoto au wanawake? Kwa sababu tunaona kuwa baadhi ya watu wanaleta waimbaji wa kike ambao gharama zao inakuwa takriban Riyaal 3000 pamoja na kuzingatia kwamba kunatokea kudensi na harakati ambazo sio katika desturi zetu waislamu. Vilevile kunakuwepo maneno ya nyimbo ya kiwendawazimu ambayo yamechukuliwa kutoka katika kanda za nyimbo. Je, haya ndio yamewekwa katika Shari´ah au kilichowekwa katika Shari´ah ni kinyume na hivo?

Jibu: Haya hayakusuniwa. Haya ni maovu. Dufu ambalo limewekwa katika Shari´ah kupiga ni lile ambalo linapigwa kwa upande mmoja na upande mwingine unakuwa wazi. Kuhusu matari ambayo yamefungwa [pande zote mbili] hayafai. Hii ni ngoma. Tofauti ilioko kati yake ni kwamba dufu lililofunguliwa upande mmoja sauti yake inakuwa khafifu. Ama ngoma iliofungwa inakuwa na mdundiko wa juu zaidi[1].

Nyimbo zilizowekwa katika Shari´ah zinaimbwa na wanawake. Waimbe nyimbo za kukaribisha na nyimbo zinazowapa furaha wale waliohudhuria. Ama kuhusu nyimbo mbovu na za kiwendawazimu hazifai.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/tofauti-ya-dufu-na-matari-ngoma-yasiyofaa-kupigwa-harusini/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1460
  • Imechapishwa: 10/01/2020