Nyimbo zinazofaa na zisizofaa harusini

Swali: Ni jambo limeenea katika kipindi cha mwisho katika baadhi ya sherehe za ndoa wanapita wasichana ambao wamekwishaolewa kati ya wanawake wengine huku wakiimba kwa kupunga nyimbo ambazo kwa kiasi kikubwa zinafanana na muziki. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Kilichosuniwa katika sherehe ya ndoa ni wanawake waimbe kwa sauti zao za kawaida. Sauti hizo zisiambatane na muziki, zisiimbwe kwa njia ya nyimbo za kisasa ambapo wanajikata au kuziremba sauti. Kitendo hichi hakijuzu. Wanatakiwa kuimba kwa sauti za kawaida. Hakuna neno kuambatanisha sauti hizo na dufu ambalo ameruhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kipambanuzi kati ya halali na haramu ni dufu na sauti katika ndoa.”[1]

Haifai kutumia ala za pumbao na za muziki. Wala haifai kuweka rekodi.

[1] Ahmad (15451).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 45
  • Imechapishwa: 28/05/2021