Hawataki tukosoea wala tusifu. Wanataka tuwe kama kondoo wanaomfuata tu mchungaji na kwamba tumfuate yule anayekuja na pesa nyingi. Hayo ndio yaliyowapitikia watu hawa huko Swan´aa´. Mwanzoni walimfuata ´Abdullaah as-Sabt na kundi lake. Wakati Suruuriyyuun walipokuja na pesa nyingi wakaingia badala yake ndani ya jahazi yake.

Ama kuhusu sisi, himdi zote ni za Allah hatupelekwi na pesa. Tunashikamana na haki. Tunasema kumwambia mtu wa Bid´ah kuwa ni mzushi hata kama atachukulia vibaya na tunasema kumwambia Sunniy kuwa ni Sunniy:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ

”Enyi walioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah pindi mnapotoa ushahidi kwa uadilifu na wala chuki ya watu isikufanyeni kutokufanya uadilifu – fanyeni uadilifu – hivyo ni karibu zaidi na uchaji Allaah.”[1]

Nimesahau kitu kimoja muhimu kinachohusiana na kujeruhi na kusifu, Jarh wa Ta´diyl; hatumwachi yule asiyekuwa na elimu juu ya haki akosoe. Ni lazima awe ni msomi na uchaji na awe na uzowefu wa kukosoa na kujeruhi. Lakini ikiwa amechuma faida kutoka kwenye vitabu vya Rabiy´ al-Madkhaliy anaweza kusema:

”Shaykh Rabiy´ bin Haadiy anasema kuwa Sayyid Qutwub ni mzushi. Shaykh Rabiy´ bin Haadiy anasema kuwa Hasan al-Bannaa ni mzushi.”

Vivyo hivyo inahusu wengine wanaolingania kwenye uzushi.

[1] 05:08

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadh’ih wa Naswaa-ih, uk. 150
  • Imechapishwa: 04/04/2017