Nini cha kufanya wazazi wakikataa kwenda Jihaad?


Swali: Kuwatii wazazi wawili ili kutoka kwenda kupigana Jihaad katika njia ya Allaah ni wajibu na kama hawakutoa rukhusa nifanye nini?

Jibu: Jihaad ambayo ni faradhi kwa baadhi ya watu (Fardhw Kifaayah) ni wajibu kupatikane ridhaa ya wazazi wawili. Kwa sababu kwenda katika Jihaad aina hii ni Sunnah na wakati ridhaa ya wazazi wawili ni wajibu. Usitangulize Sunnah juu ya wajibu. Kuna mtu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na anataka kutoka pamoja na wenye kupigana Jihaad, akamuuliza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama wazazi wake wako hai ambapo akajibu: “Ndio.” Akamwambia:

“Kapambane nao.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14819
  • Imechapishwa: 16/04/2018