Ni wajibu kwa mume kumhudumikia mke mwajiriwa?


Swali: Je, ni wajibu kwa mume kumhudumikia mke ambaye ameajiriwa?

Jibu: Ndio, kwa mujibu wa mkataba wa ndoa. Ni wajibu kwa mume kumhudumikia mke uwake kwa mujibu wa mkataba wa ndoa. Haijalishi kitu hata kama mke yuko na pesa na mshahara. Isipokuwa ikiwa kama mume alimuwekea sharti wakati wa kufunga ndoa ya kwamba hatomuhudumikia na yeye mwanamke akawa ameridhia hilo. Kwa msemo mwingine mwanamke akaridhia kuiangusha haki yake ya matumizi. Basi itambulike kuwa waislamu wanaishi kwa masharti waliyowekeana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/09-03-1436.mp3
  • Imechapishwa: 03/12/2017