Ni wajibu kwa kafiri kulipa siku zilizompita katika Ramadhaan?


Swali: Kafiri ni wajibu kulipa siku zilizompita za Ramadhaan kabla ya kusilimu kwake?

Jibu: Haimlazimu kulipa siku zilizokuwa kabla ya Uislamu wake. Kabla ya hapo maamrisho ya kufunga hayakuwa hakimgusa. Hakuwa miongoni mwa inaowalazimu swawm mpaka mtu aseme kuwa ni lazima kuzilipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/98)
  • Imechapishwa: 03/06/2017