Swali: Mtoto wa kaka yangu alipatwa na maradhi ya kansa na amefariki mwaka huu akiwa na umri wa miaka kumi na tisa ilihali bado hajatekeleza faradhi ya hajj kwa sababu ya kupatwa na maradhi haya kwa miaka tano. Je, tumhijie? Je, kuna kafara?

Jibu: Lazima tuulize kwanza: je, huyu kijana alikuwa na pesa anazoweza kuhiji kwazo? Ikiwa mambo ni hivo, basi ni lazima kumhijia. Ikiwa hana pesa, basi hija sio wajibu kwake na amekufa hali ya kuwa hajj haijamfaradhikia. Lakini ni sawa kwa yule mwenye kutaka kufanya Sunnah na kumhijia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1397
  • Imechapishwa: 11/12/2019