Ni wajibu kuitikia salamu ya kafiri?

Swali: Ni wajibu kumuitikia Salaam kafiri kama jinsi ni wajibu kumuitikia Muislamu?

Jibu: Ndio, huu ndio udhahiri wa Hadiyth. Amesema (Ta´ala):

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا

“Mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.” (07:86)

Hili ni kwa jumla.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msianze kuwapa mayahudi na manaswara salamu. Endapo watakusalimieni itikieni:

“Wa ´alaykum.”[1]

Inatakiwa kuitikia wakitoa salamu. Udhahiri ni kwamba ni wajibu.

[1] Ibn Maajah (2999). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2106
  • Imechapishwa: 01/07/2020