Ni vipi mtu atajua kuwa amepata usiku wa Qadr?

Swali: Ni vipi mtu atajua kuwa amepata usiku wa Qadr?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamba asubuhi ya siku hiyo jua linachomoza likiwa halina miale ya kuchoma. Ubayy bin Ka´b, ambaye ni Swahabah mtukufu, alikuwa akiyaona hayo katika miaka mingi. Ameliona likichomoza asubuhi ya tarehe ishirini na saba likiwa halina miale ya kuchoma. Alikuwa akiapa kwamba ni usiku wa tarehe ishirini na saba. Hii ndio alama.

Lakini usawa ni kuwa unaweza kujitokeza wakati mwingine. Unaweza kujitokeza tarehe ishirini na saba kwa miaka kadhaa, miaka mingine unaweza kujitokeza tarehe ishirini na moja, tarehe ishirini na tatu, tarehe ishirini na tano na tarehe nyenginezo. Anayetaka kuchukua salama zaidi ajitahidi katika nyusiku zote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/27442/%D8%B9%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%A7%D8%AA-%D9%84%D9%8A%D9%84%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%AF%D8%B1
  • Imechapishwa: 14/05/2020