Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya usahali juu ya fatwa? Nimeona baadhi ya ndugu pindi wanapoulizwa juu ya jambo fulani ima waende kwenye intaneti au wanukuu fatwa juu ya hili na lile. Kwa masikitiko makubwa hawajui kuwa fatwa wakati mwingine inakuwa maalum juu ya hali ya yule muulizaji. Unasemaje juu hili?

Jibu: Fatwa ni kumtilia Allaah saini, kama alivosema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika ”I´laam-ul-Muwaqqi´iyn ´an Rabb-il-´Aalamiyn”. Fatwa ni kumtilia Allaah saini kwamba amehalalisha kitu kadhaa au ameharamisha kitu kadhaa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [aina zote] na ukandamizaji bila ya haki. Na [ameharamisha] kumshirikisha Allaah kwa ambayo hakukiteremshia mamlaka na kuzungumza juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[1]

Fatwa ni kumsemea Allaah. Ikiwa ananukuu fatwa sahihi iliyojengwa juu ya Qur-aan, Sunnah na wanachuoni kwa hali ya kwamba ana uhakika nayo na ameifahamu hakuna neno kwa sababu ni kufikisha elimu. Ama kusimulia tu tetesi au kuwanukuu watu wasiokuwa na upeo wa kutoa fatwa ni jambo ambalo mtu hatakiwi kulipupia. Hakuna neno mtu akamjibu mtu maswali yake binafsi akiwa na elimu. Ama fatwa zinazohusu mambo ya kijamii na majanga zinatakiwa kutumwa katika baraza la fatwa wazijibu:

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا

“Linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wale wenye madaraka kati yao basi wale wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua.Lau si fadhila za Allaah juu yenu na rehema Zake basi hakika mngelimfuata shaytwaan isipokuwa wachache tu.”[2]

Fatwa zinazohusu jamii na majanga zinatakiwa kurudishwa katika idara ya fatwa na zisijibiwe vovyote.

[1] 07:33

[2] 04:83

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/15723
  • Imechapishwa: 21/06/2019