Ni nani mwenye haki ya kutazama barnamiji zilizopinda?

Swali: Hivi sasa watu wengi wanatoa fatwa kwenye TV na tumekuwa ni wenye kusikia Fataawaa ambazo tulikuwa hatuzisikii kutoka kwa wanachuoni wetu. Fatwa hizi ima ni zenye kuchukulia mambo kiurahisi au ziko dhidi ya watawala. Ni ipi nasaha zako kwa wale wenye kuzisikiza?

Jibu: Ninawanasihi kutahadhari na chaneli na Fataawaa hizi. Mzisitazame. Isipokuwa tu yule ambaye anataka kuziraddi na kubainisha ubatilifu wake. Vinginevyo haijuzu kuzitazama. Zinaweza kumuathiri yule mtazamaji na ´Aqiydah yake na khaswa ikiwa yule mzungumzaji anaonekana kuwa ni msomi na ni mwenye akili. Inakuwa ni jambo lenye kuathiri zaidi. Ni mtihani bila ya shaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 24/05/2018