Ni lini inaswaliwa swalah ya Dhuhaa?

Swali: Nawaona baadhi ya ndugu ambao wanaharakia kuswali Sunnah ya Ishraaq punde tu jua likishazama. Je, kitendo chao hichi ni sahihi? Ikiwa si sahihi ni lini inaswaliwa? Ningependelea, ee muheshimiwa Shaykh, unitajie hayo kwa dakika ili mtu awe juu ya ubainifu kutokana na jambo lake.

Jibu: Swalah ya Dhuhaa imesuniwa kila siku. Uchache wake ni Rak´ah mbili. Kumepokelewa Hadiyth nyingi juu yake. Wakati wake unaanza pale jua linapochomoza kwa kiasi cha mkuki kwa yule mwonaji, ambapo ni karibu robo saa kuanzia pale linapochomoza. Wakati wake bora ni pale jua linapokuwa kali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya wenye kurejearejea [kwa Allaah] ni pale jua linapokuwa kali.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Maana yake ni pale jua linapokuwa kali juu ya watoto wa ngamia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/397)
  • Imechapishwa: 12/11/2021