Ni lazima kwa mwanamke kutafuta elimu


Kama ilivyo kwa wanamme mwanamke ana jukumu juu ya matendo yake. Kwa hivyo ni lazima kwake kujifunza yale ambayo yanamlazimu kufanya ili aweze kutekeleza mambo yake ya wajibu kwa yakini.

Kama yuko na baba, kaka, mume au mwanamme mwengine ambaye hairuhusu kwake kumuoa ambaye atamfunza mambo ya wajibu na namna atakavyoyafanya, basi inatosha. Vinginevyo anapaswa kuuliza na kusoma. Jambo la kwanza anatakiwa kuhakikisha anasoma kutoka kwa mwanamke mwenzake. Akikosekana mwanamke, basi aende kwa wanamme watuwazima na amsomeshe. Hata hivyo asiketi nao faragha. Katika hali hiyo mwanamke ajifunze yale ambayo ni lazima na si zaidi ya hapo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin al-Jawziy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-un-Nisaa’, uk. 12
  • Imechapishwa: 16/04/2020