Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke ambaye hakujisitiri kukaa peke yake nyumbani na ndugu yake mwanaume na binadamu yake ambaye kishabaleghe? Hoja yake ni kwamba wamekulia pamoja tokea utotoni.

Jibu: Haijuzu. Mwanamke ambaye kishabaleghe ni lazima kwake kujisitiri hata kama amekuwa pamoja na mwanaume. Hili halimtakasi yeye kujivua mbele yake, kwa kuwa sio Mahram wake. Asivue Hijaab isipokuwa tu mbele ya Mahram zake. Huyu sio Mahram yake. Hawi Mahram wake kwa vile tu wamekulia pamoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 24/05/2018