Swali 778: Kuna mwanaume alimuoa mwanamke wa Kiislamu mwenye kuonyesha mapambo. Akampa mawaidha ya kulazimiana na Shari´ah ya Allaah na khaswa jambo linalohusiana na Hijaab. Hivyo akalazimiana na baadhi ya maamrisho kama swalah na akakataa Hijaab. Mume achukue msimamo gani juu yake? Ni lazima kwake kumtaliki au hapana? Ikiwa sio lazima kwake kumtaliki mume anapata madhami ya yeye kuonyesha mapambo yake?

Jibu: Ni lazima kwake mume kumwamrisha Hijaab. Kwa sababu Hijaab ni kitu cha lazima. Atatue jambo hilo mpaka ahakikishe amemvisha Hijaab. Mwanaume ndiye mchungi wa nyumba yake na ataulizwa juu ya kile alichokichunga. Miongoni mwa yale aliyochungishwa ni mke wake. Muda wa kuwa atamcha Allaah katika jambo hilo na akawa na subira basi Allaah atamsahilishia jambo lake na kumbarikia matendo yake. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا

“Yeyote anayemcha Allaah atamjaalia wepesi katika jambo lake.”[1]

[1] 65:04

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 304