Ni lazima kurudisha kitu ulichookota midhali unamjua mwenye nacho

Swali: Mimi nina miaka kumi na nne. Nimeokota Riyaal 100 zilizoanguka kwenye njia na kumeandikwa juu yake mwenye nazo ambapo nikazichukua. Je, nizirudishe kwa mwenyewe?

Jibu: Inatambulika kuwa ni wajibu. Ni wajibu kwa mwenye kuokota kilichopotea na akamjua mwenye nacho amfikishie nacho. Ima amwagizie nacho au amfikishie nacho. Ni lazima kufanya hivo. Masuala haya sio kama kitu kidogo. Kitu kidogo ni pale mtu anapookota kitu kidogo ambacho watu hawakitilii umuhimu basi hicho ni chake. Lakini hiki kama anamjua mwenye nacho, japokuwa ni peni moja tu… ni wajibu kulitambua hili. Ukiokota kitu cha mtu unayemjua, basi usianze kufikiria kama ni kikubwa au ni kidogo. Haijalishi kitu hata kama ni Riyaal 1. Katika hali hiyo ni wajibu kumpa nacho au angalau kwa uchahe umjuze nacho na yeye atakuja kukichukua.

Kwa ajili hii tunamwambia ndugu huyu ambaye ameokota pesa na anamjua mwenye nazo, basi ni wajibu kwake kumfikishia mwenye nazo. Pia yeye mwenyewe anaweza kwenda na kumpa nazo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1179
  • Imechapishwa: 09/07/2019