Ni lazima kunuia kwanza ili mtu apate kufuta juu ya khofu na soksi?

Swali: Ili mtu apate kufuta juu ya soksi ni sharti anuie kupangusa juu yake na vilevile anuie muda wa kufuta?

Jibu: Nia hapa sio jambo la wajibu. Hiki ni kitendo hukumu yake imefungamanishwa na kule tu kupatikana kwake. Hakuhitajii nia. Ni kama mfano iwapo atavaa nguo yake haikushurutishwa anuie kufunika vile viungo vyake visivyotakiwa kuonekana ili aweze kuswali nayo. Haikushurutishwa katika kuvaa soksi anuie kupangusa juu yake na wala kuweka nia ya muda wa kupangusa. Akiwa ni msafiri ana muda wa siku tatu. Ni mamoja amenuia au hakunuia. Akiwa ni mkazi ana muda wa mchana mmoja na usiku wake. Ni mamoja amenuia au hakunuia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/165)
  • Imechapishwa: 02/07/2017