Swali: Ni zipi fadhilah zinazopelekea kuamrisha mema na kukataza maovu kwa mmojammoja na kundi?

Jibu: Hapana shaka kwamba kuamrisha mema na kukataza maovu ni lazima kwa baadhi ya watu. Wapo wanachuoni waliolifanya kuwa nguzo ya sita ya Uislamu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu.”[1]

Maana yake ni kwamba ni lazima kwa Ummah wasimame na wajibu huu. Kukipatikana kikundi cha watu chenye kusimama na wajibu huu basi madhambi yanadondoka kwa wengine. Vinginevyo Ummah mzima unapata madhambi. Ni lazima kukemea maovu. Wale wenye kusimama na kazi hiyo wana fadhilah kubwa. Kwa sababu wamedondosha madhambi na wajibu kutoka kwa Ummah mzima.

[1] 03:104

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 17/08/2019