al-Bahrayniy amesema:

“Rabiy´ al-Madkhaliy amesema katika “al-Majmuu´ al-Waadhwih”: “Hapa nitakutajieni baadhi ya mifano kufanana baina ya wao na Raafidhwah:

1- Wana unafiki wa hali ya juu. Raafidhwiy anakubali kuwa ni Ja´fariy na baadhi ya misingi na I´tiqaad batili anayoamini. Lakini watu hawa hawakubali kuwa ni Haddaadiyyah. Hawakubali kitu katika misingi yao na yale yaliyomo vifuani mwao.” Uk. 480.

al-Bahrayniy hakujadili kitu katika mfanano huu. Hii ina maana gani? Hawezi kupinga unafiki huu wa khatari. Ni vipi ataweza kuwatetea watu wenye kujificha na wanatukana kwenye giza? Hakuna anayewajua. Mmoja wao anatukana na kusema uongo chini ya jina “Fakkaariy”. Mwingine anajiita “al-Mufarriq”. Mwingine “Khaalid al-´Aami”. Mwingine “as-Suhaymiy al-Athariy”. Wengine wana majina yasiyojulikana. Muulize ni kwa nini aliruka mfanano wa tatu na wa nne na hakuyataja na wala hakuyajadili. Niliandika:

“Kufanana kwa pili: Uhalisia wao na tovuti yao http://www.alathary.net/ ina usiri mkubwa. Hakuna kundi lolote linaweza kulinganishwa na wao kwa vile wanaandika chini ya majina yasiyojulikana na yenye kuibwa. Mmoja wao akifariki anapotea hewani. Kwa kitendo kama hichi wamewapiku hata Raafidhwah. Angalau Raafidhwah wanajulikana. Vitabu vya kihistoria na vyenye kujeruhi na kusifu vimejaa majina ya Raafidhwah na hali zao hata kama wanatumia unafiki na stara ambapo sehemu kubwa ya hali zao hazijulikai.”

Ni nani katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah anaweza kutueleza al-Mufarriq, al-Fakkaariy, Khaalid al-´Aamiy, as-Suhaymiy al-Athariy na watu wengine wasiojulikana ni kina nani? Ni kutoka katika nchi gani? Ni kutoka katika kabila gani? Wamekhitimu wapi? Wamesoma chini ya wanachuoni wepi?

Kuwatolea ushahidi watu hawa na mfano wao kwamba ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah si ni mfano wa ushahidi mchafu na ushahidi mkubwa wa uongo?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 09/10/2016