Ni ipi hukumu ya picha za viumbe wenye roho wanazochora wanafunzi mashuleni?

Swali: Vipi kuchora kwa mkono?

Jibu: Kuchora kwa mkono ni haramu. Bali ni dhambi kubwa. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Mtu halaaniwi isipokuwa kwa dhambi kubwa. Haijalishi kitu picha hiyo imechorwa ili kupima uwezo na upeo wa mwanafunzi au imechorwa kwa sababu nyingine. Yote hayo ni haramu. Lakini ikiwa kutachorwa baadhi ya viungo vya mwili kama vile mkono peke yake au kichwa peke yake hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/285)
  • Imechapishwa: 03/07/2017