Ni ipi hukumu ya mwanamke kufunika uso wake kwa wasiokuwa Mahram zake?


Swali 1029: Ni ipi hukumu ya mwanamke kufunika uso wake kwa wasiokuwa Mahram zake?

Jibu: Sunnah za kinabii zimefahamisha juu ya ulazima wa mwanamke kufunika uso wake mbele ya wasiokuwa Mahram zake. Kutokana na Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:

“Wapanda farasi wanaume walikuwa wakitupitia na sisi tuko kwenye Ihraam pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanapotujongelea, kila mmoja wetu anateremsha mavazi yake ya juu, Jilbaab, usoni mwake. Wanapokuwa wameshapita, tunajifunua tena.”

Dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah kuhusu mwanamke kufunika uso wake mbele ya wasiokuwa Mahram zake ni nyingi. Napendekeza kwako dada muislamu kusoma kitabu “al-Hijaab wal-Libaas fiys-Swalaah” cha Ibn Taymiyyah, kitabu “al-Hijaab” cha Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, kitabu “as-Swaarim al-Mash-huur ´alaa al-Muftiyniyna bis-Sufuur” cha Shaykh Hamuud at-Tuwayjiriy na kitabu “al-Hijaab”[1] cha Shaykh Swaalih bin ´Uthaymiyn. Vitabu hivi ndani yake mna yenye kutosheleza.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/category/makala/wanawake/mavazi-na-vipodozi/jumla-kuhusiana-na-vazi-la-mwanamke/al-hijaab/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 410
  • Imechapishwa: 08/10/2019