Swali: Ni ipi swawm ya kuunganisha? Imesuniwa?

Jibu: Swawm ya kuunganisha ni mtu kutofungua kwa siku mbili na hivyo akaunganisha kufunga kwa muda wa siku mbili kwa kufululiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameikataza na akasema:

“Anayetaka kuunganisha basi aunganishe mpaka muda wa kabla kuingia alfajiri.”[1]

Kufunga mpaka kipindi hicho ni kwa njia ya kujuzu. Haina maana kwamba imesuniwa kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekokoteza kufanya haraka kukata swawm:

“Watu hawatoacha kuwa juu ya kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata swawm.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1967).

[2] al-Bukhaariy (1957) na Muslim (1098).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 492
  • Imechapishwa: 29/04/2020