Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka nia katika swalah na mengineyo?

Jibu: Kutamka nia ni kitu ambacho kilikuwa hakitambuliki katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakati wa as-Salaf as-Swaalih. Ni jambo lililozuliwa na watu na hakuna haja. Kwa kuwa nia pahali pake ni moyoni. Allaah (Ta´ala) ni mjuzi wa yaliyomo katika nyoyo za waja Wake. Husimami mbele ya yule asiyejua mpaka useme kuwa unataka kutamka uliyonuia. Unataka kusimama mbele ya yule ambaye anaelewa yale yanayoning´onezwa na nafsi yako, anayaelewa mambo yako yaliyoko mbele, yaliyopita na ya sasa. Kwa hivyo kutamka nia ni miongoni mwa mambo ambayo hayakuwa yakitambulika kwa as-Salaf as-Swaalih. Ingelikuwa ni jema basi wangelitutangulia kwalo. Haitakikani kwa mtu kutamka nia, si katika swalah wala katika ´ibaadah nyenginezo, si kimoyoni wala kwa dhahiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/442)
  • Imechapishwa: 23/07/2017