Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kati ya nguzo?

Jibu: Kuswali kati ya nguzo inafaa wakati wa dhiki ya nafasi. Ama kukiweko nafasi ya kutosha haifai kuswali kati ya nguzo. Kwa sababu kufanya hivo kunakata safu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 311
  • Imechapishwa: 06/05/2020