Ni ipi hukumu ya kujipaka poda?


Swali: Ni ipi hukumu ya poda ambayo wanaweka huweka kwenye nyuso zao kwa sababu ya kujipamba?

Jibu: Poda inahitajia upambanuzi. Ikiwa inaupamba uso na wakati huohuo haidhuru uso na wala haisababishi kitu basi haina neno wala ubaya. Lakini ikiwa inasababisha kitu kama vile viupele vyeusi au inasababisha madhara mengine, basi itakatazwa kutokana na madhara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/497)
  • Imechapishwa: 13/03/2021