Ni ipi hukumu ya kufanya I´tikaaf?

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya I´tikaaf?

Jibu: I´tikaaf ni mtu kulazimiana na msikiti kwa ajili ya kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ili apwekeke kutokamana na watu kwa ajili ya kujishughulisha na kumtii Allaah na kupata nafasi kwa ajili ya hilo. I´tikaaf inafanywa katika misikiti yote. Ni mamoja iwe ni msikiti unaoswaliwa ijumaa au msikiti usioswaliwa ijumaa. Lakini bora ni kufanya I´tikaaf katika msikiti unaoswaliwa ijumaa ili mtu asilazimike kutoka kwa ajili ya kuswali ijumaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/155)
  • Imechapishwa: 15/06/2017