Ni ipi hukumu maamuma akiacha kitu cha wajibu kwa kusahau?

Swali 30: Ni ipi hukumu maamuma akiacha kitu cha wajibu kwa kusahau?

Jibu: Ikiwa ameswali na imamu tokea kuanza kwa swalah, basi yeye ni mwenye kumfuata imamu wake. Hakuna kinachomlazimu. Na ikiwa amesahau nyuma ya imamu wake na alikuja amechelewa au akasahau katikati yake, basi asujudu Sujuud ya kusahau baada ya kulipa yale yaliyompita.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 36
  • Imechapishwa: 05/11/2018