Ni haramu kuacha kufunga kwa ajili ya kazi

Swali: Inajuzu kula kwa yule ambaye kazi yake ni ngumu na kufunga kunamtia uzito?

Jibu: Ninavyoonelea ni kwamba kuacha kufunga kwa ajili ya kazi ni haramu na wala haijuzu. Ikiwa hawezi kufunga na kufanya kazi vyote viwili kwa pamoja basi achukue likizo katika Ramadhaan ili aweze kufunga. Kwa kuwa kufunga Ramadhaan ni nguzo ya Uislamu na wala haijuzu kuiacha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/92)
  • Imechapishwa: 31/05/2017