Nenda katika kituo cha Kiislamu nchini mwako

Swali: Dada huyu muulizaji kutoka Uholanzi anasema kwamba alikuja mposaji kumposa na wazazi wake wakamkatalia kwa hoja eti anaishi mbali pamoja na kuzingatia kwamba umbali wenyewe ni wa saa moja. Msichana huyu afanye nini katika hali kama hii ilihali anataka kuolewa na kuichunga nafsi yake kutokamana na machafu katika nchi ya kikafiri?

Jibu: Aende katika kituo cha Kiislamu katika nchi yake na wao wataangalia jambo lake.

  • Mhusika: Imam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18340
  • Imechapishwa: 15/10/2021