Swali: Ni ipi hukumu ya kuwatembelea ndugu ikiwa wanadhihirisha wazi madhambi na wanachezea shere kitu katika dini?

Jibu: Wanatakiwa kunasihiwa. Awatembelee kwa ajili ya kuwanasihi. Huyu ndiye ndugu ambaye ana haki zaidi ya kutembelewa. Mlinganie kwa Allaah, umnasihi, umwamrishe mema na umkataze maovu. Allaah (Ta´ala) amesema akimwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ

“Na waonye jamaa zako wa karibu.” (ash-Shu´raa 26:214)

Wao ndio wana haki zaidi ya kunasihiwa. Kwa hivyo watembelee na uwanasihi. Haifai kwako kunyamaza. Ikiwa utawaendea, ukawanyamazia na ukakaa pamoja nao basi na wewe unashirikiana nao katika madhambi. Lakini keti pamoja nao kwa njia ya kuwanasihi, kuwalingania na kuwalekeza kwa ulaini na urafiki.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 05/10/2019