Ndio maana kulingana kwa Allaah ni kitu maalum juu ya ´Arshi

Jahmiyyah, Mu´tazilah na Haruuriyyah wamesema maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

Mwingi wa huruma amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

maana yake kwamba Amelingana na ameimiliki na kwamba Allaah (´Azza wa Jall) yuko kila mahali. Wanapinga Allaah (´Azza wa Jall) kuwa juu ya ´Arshi, kama wanavyosema Ahl-ul-Haqq. Wanaonelea kuwa kulingana ni kuweza.

Mambo yangelikuwa hivo wanavyosema basi kusingelikuwa tofauti yoyote kati ya ´Arshi na ardhi ya saba, kwa kuwa ana Allaah umiliki juu ya kila kitu.

Endapo kulingana kwa Allaah juu ya ´Arshi maana yake ingelikuwa ni kutawala – kwani Yeye si ana utawala juu ya kila kitu – basi kulingana Kwake kungelikuwa juu ya ´Arshi, mbingu, ardhi, mashamba ya mitende, takataka na watu, kwa kuwa ana utawala juu ya kila kitu. Ikiwa Allaah ana utawala juu ya kitu, basi haijuzu kwa muislamu yeyote yule kusema kuwa Allaah (´Azza wa Jall) amelingana juu ya mashamba ya mitende na vyoo. Ametakasika Allaah kutokamana na kitu kama hicho. Kwa hiyo ingelikuwa haijuzu kutofautisha ´Arshi na kulingana kwa kuwa Allaah ana utawala juu ya kila kitu. Kwa ajili hiyo kulingana ni maalum na ´Arshi na si chengine.

[1] 20:05

  • Mhusika: Imaam Abul-Hasan ´Aliy bin Ismaa´iyl al-Ash´ariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibaanah, uk. 34
  • Imechapishwa: 14/04/2017