Ndio maana al-Khaliyliy amechagua tafsiri ya kusubiri


Pili: Madai ya al-Khaliyliy Ibaadhwiy kwamba amechagua hii tafsiri[1] kwa sababu Aayah inapingana na dalili zinazokanusha kuonekana kwa Allaah ambazo ni za kukata kabisa (Qatw´iyyah).

Mwenendo huu ni wa kigeni na ni wa ajabu kabisa kutoka kwa al-Khaliyliy.

Tunamuuliza ziko wapi dalili za kukata kabisa ambazo zinakanusha kuonekana kwa Allaah Aakhirah, katika uwanja wa Qiyaamah na baada ya waumini kuingia Peponi? Tunamraddi kwa njia mbili:

Mosi: Ibaadhwiy! Hukuleta dalili hata moja wala Aayah ambazo ni Muhkam kutoka katika Qur-aan wala upokezi uliyosimama kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Swahiyh au dhaifu ili utilie nguvu uliyoyataja. Ulichotaja ni utatazi na udanganyifu. Ulichofanya ni kutaja dalili za wazi ambazo zinakanusha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuona Mola wake usiku wa Israa´ na Mi´raaj. Muonekano huu unahusiana na duniani na sio Aakhirah. Ahl-us-Sunnah wote wanakanusha kuwa Allaah ataonekana hapa duniani. Huu ndio utatizi na udanganyifu wenyewe kutaka kufanya dalili zinazokanusha kuonekana kwa Allaah duniani juu ya kukanusha kuonekana kwa Allaah duniani na Aakhirah.

Pili: Unarudisha dalili za Qur-aan kwa tafsiri batili. Unachagua maana moja ya kilugha na kufasiri kwayo Aayah kwa ajili tu ya kufuata matamanio yako. Huu ni mfumo ambao umepewa mtihani kwao na wamepewa mtihani kwao watu wapumbavu ambao wanadanganyika kwa maneno ya kupambapamba na kugeuza uhakika wa mambo.

[1] Kwamba ”ilaa Rabbihaa an-Naadhwirah” maana yake ni wanamsubiri Mola wao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 80
  • Imechapishwa: 14/01/2017