Ndio Hadiyth ni Swahiyh


Swali: Hadiyth isemayo: “Ummah huu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” ni Swahiyh?

Jibu: Ndio, ni Swahiyh kwa njia zake zote. Kwa sababu imepokelewa kwa njia nyingi ambazo zimetajwa na wanachuoni. Kwa njia zake zote ni Hadiyth Swahiyh.