Nchi ya Kiislamu kwa mujibu wa Ibn Baaz

Swali: Miji mingi ya Kiislamu ina mambo ya kishirki na wanawaabudu majengo ya waja wema. Je, miji hii inaitwa kuwa ni ya “Kiislamu” au hapana?

Jibu: Inategemea. Ikiwa nembo za kikafiri ndio zilizoenea kwa wingi zaidi basi ni miji ya kikafiri. Ikiwa nembo za Kiislamu ndio zilizo kwa wingi basi hiyo ni miji ya Kiislamu. Kinachozingatiwa ni kile kilichoenea na kushinda zaidi.

Swali: Wanaswali, wanafunga na kuna misikiti.

Jibu: Kunatazamwa kile kilichoea zaidi. Nchi ina hukumu kutegemea kile kilichoenea zaidi.

Swali: Wakazi wengi ni waislamu, jina ni la Kiislamu.

Jibu: Ikiwa chenye kuonekana zaidi ni jina la Uislamu, wema na mengine katika nembo za Uislamu basi ni nchi ya Kiislamu japokuwa mtawala atakuwa kafiri.

Swali: Nchi itakuwa ya Kiislamu?

Jibu: Ndio, ndio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh-il-Maraam (2) https://youtu.be/bgz0JX6ynJA
  • Imechapishwa: 30/06/2019