Swali: Ikiwa maovu anayoona mwanamke muumini ni mchanganyiko na wanawake kutojisitiri. Ni vipi atawanasihi?

Jibu: Unatakiwa uwanasihi na kumwambia dada yako kwa ajili ya Allaah ya kwamba ni wajibu kwake kutochanganyika na wanaume, kutovaa vibaya na kutilia umuhimu suala la kujisitiri mbele ya wanaume ambao sio Mahaarim zake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

“Mnapowauliza basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.” (33:53)

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazihifadhi tupu zao na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao na wasionyeshe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao [dada zao wa kiislamu], au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao -na tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, mpate kufaulu.” (24:31)

Mtajie Aayah na Hadiyth zinazohusiana na hiyo mada na ambazo ndani yake kumetajwa kwa wazi kinachotakikana na zinatahadharisha kwenda kinyume na Shari´ah safi. Wawekee wazi vilevile dada zako kwa ajili ya Allaah ya kwamba lililo la wajibu kwetu sote ni kutahadhari na yale aliyoharamisha Allaah, kusaidiana katika wema na uchaji Allaah, kuusiana kwa yaliyo ya haki na kusubiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/234)
  • Imechapishwa: 03/07/2017