Namna atakvyojitwahirisha hedhi ambaye amefanyiwa operesheni mguuni

Swali: Mwanamke huyu alilazwa hospitalini baada ya kufanyiwa operesheni mguuni mwake na kipindi hicho alikuwa na ada ya mwezi. Akasafika akiwa bado amelazwa hospitali na hakuweza kujisafisha kutokamana na hedhi. Matokeo yake akafanya Tayammum na akaswali vipindi vingi vya swalah. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Ikiwa hakuweza kuoga basi Tayammum inatosheleza. Lakini kama aliweza kuoga sehemu iliyobaki ya mwili wake, mbali na mguuni mwake, basi alitakiwa kuosha kichwa chake na sehemu nyingine ya mwili wake iliyobaki tukiondoa mguu ambao alifanyiwa operesheni.

Kimsingi ni kwamba ni lazima kwake kuoga. Lakini hakuna neno ikiwa kuoga kwake kutampelekea katika mambo yatakayomdhuru kutokana na majeraha au madaktari wakamshauri asitumie maji kile kipindi cha matibabu kwa sababu maji yanamdhuru. Katika hali hiyo Tayammum yake ni sahihi na swalah yake ni sahihi.

Lakini kama ni mguu peke yake anatakiwa kuuepusha na maji na asiuoshe. Lakini atatakiwa kuosha sehemu nyingine ya mwili iliyobaki kutokamana na hedhi na janaba. Ikiwa maji hayamdhuru isipokuwa mwili peke yake, basi itambidi azirudi swalah alizoswali baada ya kuoga. Mguu ukiwa umevishwa bendeji basi atafuta juu yake yote na itamtosha kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4347/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B7%D9%87%D8%B1%D8%AA-%D9%88%D8%AA%D8%B9%D8%B0%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%BA%D8%B3%D9%84-%D9%84%D8%AC%D8%B1%D8%A7%D8%AD%D8%A9
  • Imechapishwa: 05/06/2020