Nadhiri ina matamshi maalum?


Swali: Ni matamshi yepi ya nadhiri ambayo ni lazima kwa mtu kuitimiza? Je, inatangulizwa kwa kiapo au ni pale ambapo mtu anajilazimisha kufanya kitu fulani?

Jibu: Nadhiri haina matamshi maalum. Bali kila neno linalojulisha mja kujilazimisha kitu kwa ajili ya Allaah basi hiyo ni nadhiri. Yakiambatanishwa na kiapo basi inakuwa kiapo na nadhiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (13) http://binothaimeen.net/content/6770
  • Imechapishwa: 04/02/2021