Mwenye ugonjwa wa ini na Ramadhaan


Swali: Kuna mgonjwa aliye na maradhi ya ini na daktari amemwamrisha kula kwa ajili ya kutumia dawa na kutokana na udhaifu wa ini na inasemekana kuwa anaweza kutembea kuelekea msikitini na kwenda hospitali. Je, anaruhusiwa kula na hali ni kama ilivyotajwa?

Jibu: Mambo yakiwa kama alivyoeleza muulizaji ya kwamba ana ugonjwa kwenye ini lake na kwamba daktari amemwamrisha kuacha kufunga, daktari huyo akiwa ni mwaminifu, mwenye amana na mzoefu katika kazi yake basi maamrisho yake yanazingatiwa kwa anavyojua kutokana ni maradhi gani yanayoweza kufunga na ni yepi yasiyoweza. Lakini hata hivyo ni wajibu kwake kulipa zile siku alizokula baada ya kuwa na uwezo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/194-195)
  • Imechapishwa: 06/06/2017