Swali: Vipi kuhusu kuswali nyumbani?

al-Fawzaan: Swalah ya faradhi au ya Sunnah?

Muulizaji: Ya faradhi.

Jibu: Haijuzu kuswali nyumbani isipokuwa kwa udhuru wa Kishari´ah. Swalah ya mkusanyiko ni wajibu. Swali pamoja na wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusikia adhaana na asiiendee, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Kukasemwa: “Ni udhuru upi?” Akasema: “Ni khofu au maradhi.”

Kwa hivyo haijuzu kuacha swalah ya mkusanyiko ilihali unaweza kuhudhuria.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2017