Mwanaume kuoa baada tu ya mke wake kufa


Swali: Akifa mke wa mtu inajuzu kwake kuoa mwanamke mwengine tokea kufa kwake kwa mwezi mmoja, chini ya hapo au zaidi  ya hapo? Wapo baadhi ya maimamu wanaosema kuwa haifai isipokuwa mpaka kupite miezi mitatu. Nimeshangazwa na jambo hili; ni sahihi au hapana?

Jibu: Mke wa mwanaume akifa inafaa kwake kuoa pale anapotaka. Aliyoyataja hayana msingi wowote. Bali ni batili.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/27-28)
  • Imechapishwa: 20/08/2017