Swali 05: Mfanyakazi ambaye anakuwa mbali na mke wake kwa muda mrefu anapata dhambi au adhabu pamoja na kuzingatia kwamba yuko katika hukumu ya kazi yake na wala hafanyi upungufu juu ya familia yake mbali na kutomuona tu.

Jibu: Mwanaume akiwa mbali na mke wake kwa ajili ya kutekeleza wajibu unaomuhusu yeye au familia yake au Ummah, hapati dhambi wala adhabu. Akighaibika kwa muda mrefu pasi na udhuru wala kutekeleza wajibu na [mke] akaridhika juu ya hilo, hapati dhambi pia wala adhabu. Mke asiporidhia anapata dhambi. Mwanaume huyu anastahiku kuadhibiwa.  Kwa sababu amezembea juu ya haki za mke za kindoa ingawa atakuwa ni  mwenye kutekeleza wajibu wake upande wa maisha, mavazi, makazi na malazi. Mwanamke huyu ana haki za kuomba haki zake za kindoa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (19/338)
  • Imechapishwa: 24/06/2019