Mwanamke kuhiji bila Mahram au na kundi la wanawake wenzake

Swali: Mwanaume na mwanamke watuwazima wako na mfanyakazi wa kike ambaye anataka kwenda kuhiji. Amekazania pamoja na kwamba hana Mahram. Wamembukia katika moja ya mashirika ya nchi. Je, sisi tunapata dhambi kwa kufanya hivo pamoja na kwamba alikuja kwetu pia bila kuwa na Mahram? Ni vigumu kwake kuja mara nyingine pamoja na Mahram ili kutekeleza faradhi ya hajj. Tunaomba utupe fatwa na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Haijuzu kwa mfanyakazi wa kike pasi na Mahram. Haijalishi kitu hata kama atakuwa na wanawake. Haijalishi kitu hata kama wapo wanachuoni wanaosema kwamba mwanamke akiwa na wanawake wenzake na wakati huohuo mwanamke huyo akawa ni mwaminifu, basi hakuna neno akahiji. Lakini tukitazama Hadiyth Swahiyh ambapo siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoa Khutbah na akasema:

“Mwanamke asisafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.” Mwanaume mmoja akasimama na akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Mke wangu ametoka ameenda kuhiji na mimi tayari nimekwishaandikwa katika vita fulani.” Akamwambia: “Nenda zako ukahiji na mke wako.”

Akamwamrisha aache kwenda vitani na akahiji na mke wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuuliza kama yuko na wanawake wenzake, kama ni mwaninifu, kama bado ni msichana, kama ni mzee, kama ni mrembo, kama ni mbaya na mengineyo. Hakupambanua. Inatambulika kwamba miongoni mwa kanuni za wanachuoni ni kwamba kuacha kupambanua mahali ambayo kunaweza kupatikana tafsiri nyingi, basi kunapelekea manzilah ya ujumla katika maneno.

Hivyo mimi naona kuwa asimwache akaenda kuhiji. Hili ni mosi.

Pili naona kwamba wote wawili wanatakiwa kumtuliza na kumwambia kwamba hajj bado haijamuwajibikia na kwamba akikutana na Mola wake bado atakuwa amekutana Naye pasi na kuwa amefanya upungufu wowote katika nguzo ya Uislamu. Wamwambie asubiri mpaka pale Allaah atapomfanyia wepesi jambo lake kuwa na Mahram.

Ama udhuru wao kwamba amekuja pia bila Mahram ni jambo la ajabu. Wanatoa udhuru kwa maradhi mfano wake au maradhi makubwa kuliko. Kitendo chake cha kwamba alikuja bila Mahram hakimtakasii kwamba ahiji bila Mahram. Kuja kwake pasi na Mahram ni kosa. Kumetokea majanga mengi kwa sababu mfanyakazi hana Mahram nyumbani anakoishi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1196