Mwanamke atakuwa na mume wake wa mwisho

1281- Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke atakuwa na yule mume wake wa mwisho.”

Ameipokea Abu ´Aliy al-Harraaniy al-Qushayriy katika ”Taarikh Raqqah”[1] ambaye amesema:

al-´Abbaas bin Swaalih bin Musaafir al-Harraaniy ametuhadithia: Abu ´Abdillaah Ismaa´iyl bin ´Abdillaah bin Khaalid as-Sukkariy ametuhadithia: Abul-Maliyh ametuhadithia, kutoka kwa Maymuun bin Mahraan ambaye amesema:

“Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) alimposa Umm-ud-Dardaa’ ambapo akakataa na akasema: “Nilimsikia Abud-Dardaa’ akisema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke atakuwa na yule mume wake wa mwisho” au “Mwanamke atakuwa kwa yule mume wake wa mwisho.”

Mimi simtaki mwingine zaidi ya Abud-Dardaa’.”

Wanaume wa cheni ya wapokezi ni waaminifu na wenye kutambulika isipokuwa tu al-´Abbaas bin Swaalih. Sijapata wasifu wake. Watu warejee katika “al-Jarh wat-Ta´diyl”[2]

Kwa ujumla Hadiyth, kwa cheni za wapokezi zote, ina nguvu na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni sahihi.

[1] 2/39/3.

[2] Mimi mwenyewe nilirejea huko na sikupata kitu. Ibn Hibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat” (8/514).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (3/275-276)
  • Imechapishwa: 25/05/2019