Mwanamke atakiwa kufunika uso mbele ya mvulana wa miaka ngapi?

Swali: Ni lini mwanamke anafunika uso wake mbele ya mtoto mdogo wa kiume?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) hakufungamanisha hilo na mwaka maalum. Alichosema ni:

أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ

“… au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake.”[1]

Ikiwa mtoto huyu hawajali wanawake, hawawageukii na wala hataji walivyo, basi hakuna ubaya kufunua uso wako mbele yake.

Ama ikitambulika kuwa anawatazama wanawake kwa kuwatamani, hapa anakuwa mwenye kutambua kuhusu sehemu za siri za wanawake. Katika hali hiyo si halali kwa mwanamke kujifunua mbele yake. Mara nyingi mtoto aliyefikisha miaka kumi anatambua nyuchi za wanawake.

[1] 24:31

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/842
  • Imechapishwa: 19/06/2020