Mwanamke anaweka dawa ya kuzuia manii yasifike kwenye uke


Swali: Kuna mwanamke ambaye anaweka dawa wakati wa kuingiliana na mume wake ambayo inazuia manii kufika kwenye fuko la uzazi. Je, kitendo hicho ni chenye kufaa ambacho ni halali au ni haramu? Je, dawa hiyo ikibaki hapo baada ya jimaa na kusitoke kitu inafaa kwake kuswali na kufunga baada ya kuoga au haifai?

Jibu: Kuhusu swalah na swawm yake ni sahihi hata kama dawa hiyo itakuwa ndani yake. Kuhusu kujuzu kufanya hivo wanachuoni wametofautiana. Lililo salama zaidi kwake ni yeye kutofanya hivo. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/297)
  • Imechapishwa: 14/11/2017